Maduka
ya nguo ya Woolworths yenye matawi yake jijini Dar es Salaam na Arusha,
yametangaza punguzo kubwa la bei kwa bidhaa tofauti tofauti
zinazopatikana katika maduka yake.
Mkurugenzi wa fedha wa Woolworths Tanzania Samson Katemi alisema punguzo
hilo kubwa la bei ni la hadi kufikia asilimia hamsini na litadumu kwa
wiki moja kuanzia leo Jumanne.
“Lengo la Woolworths ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anaweza kumudu
kununua nguo mpya na za kisasa kwa gharama nafuu na kuachana na mitumba
na ndiyo maana huwa tunakuwa na punguzo la bei mara kwa mara,” alisema.
Mkurugenzi wa fedha wa maduka ya nguo ya Woolorths Samson Katemi,
akimkabidhi mshindi wa hivi karibuni wa droo ya mwezi Lilian William
Divas vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi laki tano. Wateja wa
Woolworths wanaofanya manunuzi kupitia kadi maalum za manunuzi
(Wrewards) wanayo nafasi ya kujishindia vocha hizo.
Katemi
alisema punguzo hili litawawezesha wateja wa Woolworths watakafanya
manunuzi katika maduka yake yaliyopo PPF Towers na Mikocheni kwa jijini
Dar es Salaam pamoja na TFA na Njiro Complex kwa jijini Arusha wataweza
kupata punguzo hilo katika bidhaa kama nguo za watoto, wanawake na
wanaume
“Kwa wateja wenye kadi maalum za manunuzi za Wrewards, watapata asilimia
10 zaidi ya punguzo. Kama mteja hana kadi ya Wrewards afike katika
maduka yetu ili aweze kuipata bila malipo na aweze kunufaika na
asilimia10 zaidi,” alieleza .
Baadhi ya bidhaa mpya zilizopo katika maduka ya Woolworths kama ambavyo
kamera yetu ilifanikiwa kuzinasa katika moja ya maduka ya Woolworths
yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Katemi
aliongeza kuwa, wateja wanaofanya manunuzi kwa kutumia kadi za Wrewards
wanayo nafasi yakuingia kwenye droo zinazofanyika kila mwezi na
kujishindia vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi laki tano ambazo
huweza kutumika ndani ya kipindi cha miezi sita.
“Katika droo ya mwezi Aprili, Lilian William Divas aliweza kuibuka
mshindi. Kila mteja anayetumia Wrewards kadi kufanya manunuzi anaweza
kuwa mshindi kama alivyokuwa Lilian,” aliongeza . Na katika droo ya
mwezi wa sita Amina Shaban na Abdul Karim Ngarama waliibuka washindi.
No comments:
Post a Comment