Usalama wa Kibiti ambako kumekuwa kukiripotiwa mauaji ya viongozi wa
vyama na serikali na raia imeelezwa kuwa ni salama tofauti na kipindi
cha nyuma ingawa bado Jeshi la Polisi litaendelea kuhakikisha kila
anayejihusisha na uhalifu anatiwa katika mikono ya sheria popote alipo.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba amesema kuwa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo mauaji ya raia yaliripotiwa kila mara lakini sasa hali imekuwa shwari:>>>”Kipindi
kilichopita ilikuwa kila baada ya siku mbili unasikia kuna tukio lakini
sasa utaona kwamba kwa muda haujasikia matukio ya aina hiyo.
“Sisi
kwenye mambo ya uhalifu hatuwaombi watu kuacha. Hatuwabemebelezi watu
kuacha uhalifu. Tunawaambia tutapambana na uhalifu na tutapambana na
wahalifu mmoja baada ya mwingine. Tutapambana nao na tutahakikisha
kwamba tunakomesha uhalifu.” – Waziri Mwigulu Nchemba.
SHARE
No comments:
Post a Comment