Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kama Prof Maji Marefu akitoa msaada wa kuwaokoa wananchi wa jimbo lake wakati wa mafuriko yaliyotokana na mvua miezi michache iliyopita.
UKITEMBELEA Jimbo la Korogwe Vijijini linaloongozwa na
Stephen Ngonyani (CCM) maarufu kama Profesa Majimarefu utaona jinsi kuna mabadiliko
makubwa ya kimaendeleo.
Mbunge huyo hayupo tayari kuona wananchi wa jimbo lake
wanapata matatizo ndiyo maana anatumia kila linalowezekana kutatua kero zao.
Kwa mfano, mwaka jana alitoa madawati 200 na kupokelewa na Mkuu
wa Wlaya ya Korogwe, Robert Gabriel.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngony'ani maarufu Proffesa Maji Marefu kulia kushoto ni Diwani wa Kata ya Kerenge wilayani Korogwe wakiwa wamebeba moja kati ya madawati 200 ambayo yalikabidhiwa na mbunge huyo kupitia Fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya shule za msingi wilayani Korogwe.
Hii yote ni kuhakikisha anaharakisha maendeleo ya wananchi wa
jimbo hilo kwa kila mwanafunzi kusoma kwa utulivu.
Si tu kusoma kwa utulivu, lakini pia kukabiliana na tatizo
hilo na kuhakikisha linaondoka. Hili nalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Jitihada za aina hiyo amezifanya maeneo mengine mengi ndani
ya jimbo lake, ikiwemo sekta za afya, elimu, miundombinu, maji na wakati
mwingine kutolea yeye mwenyewe ili kuhakikisha masuala ya jimbo lake hayabaki
nyuma.
Hata hivyo, tukio ambalo alilifanya na kuendelea kugonga
vichwa vya wananchi wengi ni pale alipojitokeza kuokoa baadhi yao wakati mvua
kubwa iliponyesha.
Mbunge huyo alishiriki kwa kuwabeba na kuhakikisha anaonesha
mfano badala ya kukaa na kuagiza.
Huyo ndiye Profesa Majimarefu ambaye anatumia nafasi yake
kuhudumia wananchi kwa ukaribu ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wake kama
mwakilishi wa wapigakura wa Jimbo la Korogwe Vijijini.
SHARE
No comments:
Post a Comment