Timu inayocheza
soka ya Marekani Dallas Cowboys imetetea umaarufu wake kama timu ya
michezo ilio na thamani ya juu kulingana na jarida la Forbes.
Hatua hiyo inaiweka United katika nafasi ya 3 kwa jumla.
Thamani ya Dallas Cowboys iliongezeka kwa asilimia 5 hadi dola bilioni 4.2 huku klabu ya mpira wa baseball New York Yankees ikiwa ya pili na thamani ya dola milioni 3.7.
Hatahivyo timu ya Los Angeles Rams ndio iliopata faida kubwa na hivyobasi kupanda kutoka timu hamsini bora hadi nafasi ya 12 baada ya thamani yake kupanda maradufu hadi dola bilioni 2.9 kufuatia hatua yao ya kuondoka St Louis mwaka uliopita.
''Kuhama huko pamoja na uwanja mpya kumesababisha kuongezeka kwa thamani ya timu za NFL'', alisema Kurt Badenhausen, muhariri mkuu katika jarida la Forbes.
Timu za ligi ya NFL zilikuwa katika nafasi ya 29 miongoni mwa timu hamsini bora isipokuwa Cincinnati Bengals, Buffalo Bills na Detroit Lions ambazo hazikushirikishwa.
Hakuna timu hata moja ya kuteleza barafuni, ama hata ile ya magari ya langalanga ya Formular one iliorodheshwa.
Orodha ya timu 10 zenye thamani ya juu duniani:
- 1. Dallas Cowboys $4.2bn (£3.26bn) American football
- 2. New York Yankees $3.7bn (£2.87bn) baseball
- 3. Manchester United $3.69bn (£2.86bn) football
- 4. Barcelona $3.64bn (£2.82bn) football
- 5. Real Madrid $3.58bn (£2.78bn) football
- 6. New England Patriots $3.4bn (£2.64bn) American football
- 7. New York Knicks $3.3bn (£2.56bn) basketball
- 8. New York Giants $3.1bn (£2.4bn) American football
- 9. San Francisco 49ers $3bn (£2.33bn) American football
- 10. Los Angeles Lakers $3bn (£2.33bn) basketball
- CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment