Floyd Mayweather na
mpinzani wake Conor McGregor waliendelea kurushiana cheche za maneno
katika siku ya pili ya kampeni ya kuuza pigano lao mnamo mwezi Agosti
mjini Las Vegas.
McGregor mwenye umri wa miaka 28 alicheza densi katika jukwaa akimkosoa Mayweather mwenye umri wa miaka 40.
Wawili hao watakutana katika piogano lka raudni 12 chini ya sheria za ndondi tarehe 26 mwezi Agosti.
Katika msururu wa kushushaiana matusi Nyota mpiganaji McGregor alimtusi kuhusu nguo aliovaa na hata kusema kuwa hawezi kusoma.
Nakaaje? McGregor aliuuliza umati, kabla ya kulekeza kidole chake kwa begi aliyobeba Mayweather. Ana miaka 40! Vaa kama umri wako, sio kubeba begi la shule katika jukwaa.
Unafanaya nini na begi la shule katika jukwaa? Huwezi hata kusoma. Mayweather aliyevalia Tisheti na kofia huk McGregor akiwa amevalia suti, alijibu.
Ni mimi ambaye siwezi kusoma? Nafanya hesabu, na natengeza fedha. Unadaiwa fedha, McGregor alimjibu, akizungumza kutoka na ripoti kwamba Mayweather aliitaka IRS mapema mwezi huu kupewa muda zaidi wa kulipa kodi ya mwaka 2015.
SHARE
No comments:
Post a Comment