Majengo ya Urusi yanayoshikiliwa na Marekani
Mazungumzo kati ya
maafisa waandamizi wa Marekani na Urusi yamemalizika mjini Washington
juu ya madai ya Moscow kutaka kurudishiwa majengo yake mawili
wanayofanyia shughuli za kibalozi yaliyokuwa yakishikiliwa kutoka Desemba
mwaka jana na utawala wa Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama.
Awali Urusi ilionya kuchukua hatua ya kulipiza kisasi iwapo vifaa katika majengo hayo vinawekwa tena. maeneo hayo yaliyokuwa yakishikiliwa na Marekani kutokana na madai kuwa yalikuwa yakitumiwa kwa shughuli za kiintelijensia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov ameishutumu Marekani kwa kile alichokiita ''..Wizi wa wazi''
Hali ya kisiasa nchini Marekani imekuwa mbaya katika wakati pia uchunguzi juu ya Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Rais nchini humo ukiendelea
SHARE










No comments:
Post a Comment