TRA

TRA

Wednesday, July 5, 2017

MAONESHO YA SABASABA 2017; BABA AMSAJILI MWANAE WA MIAKA 18 NA MPANGO WA "WOTE SCHEME" WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BWANA Sukulu Mageta akiwa na mkewe Diana wote wajasiriamali wakiwa na watoto wao, Msuya S Mageta (18) na Ng'washi S Mageta, aliamua kutumia muda wake mchache kutembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF, ili kujua nini hasa anachoweza kufaidika nacho endapo atajiunga na Mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Jannet Ezekiel ndiye aliyekuwa na jukumu la kutoa "darasa" kuhusu faida za kujiunga na PPF kupitia mpango wa WOTE SCHEME, ambao ni maalum kwa wanachama wanaojiunga kwa uchangiaji wa hiari, mpango unaowahusu wajasiriamali, mama lishe, bodaboda na mgtu yeyote anayefanya kazi ya kumuingizia kipato na uwezo wa kuchangia kila mwezi angalau shilingi elfu 20.
Bi Jannet aliieleza familia hiyo kuwa mwanachama wa mpango wa wote scheme, atafaidi Mafao mbalimbali yakiwemo, Mafao ya afya,  Mkopo wa Elimu, na Mafao mengine mengi. Baada ya kupatiwa elimu hiyo, Bw. Sukulu aliamua kumuandikisha kijana wake wa mika 18 Msuya S. Mageta kujiunga na mpango huo wa WOTE SCHEME, kwa lengo la kujiwekea akiba ili afaidike na Mkopo wa elimu.
 Bi Jannet Ezekiel, (kushoto), akimkabidhi fomu ya kujiunga na Mpango wa WOTE SCHEME, kijana Msuya S. Mageta. Katikati ni baba mzazi wa Msuya, Bw. Sukulu Mageta
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PPF, Bi. Pauline Msanga, akichapa kazi
 Afisa Msaidizi Huduma kwa Wateja, Bw. Mohammed Siaga, akichapa mzigo
 Afisa Mtafiti wa PPF, Bi.Elaine Maro, (kulia), akimpokea kwa bashasha mwanachama huyu aliyefika kupatiwa taarifa zamichango yake
 Baada ya muda mchache mwanachama huyo anapata taarifa yake na ufafanuzi pia
 Afisa Mafao wa PPF, Bi. Tulla Mwigune, (kushoto), akimpatia maelezo mwanachama huyu aliyefika kwenye banda la Mfuko huu

 Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia WOTE SCHEME, Bw.Martin Mtenga.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger