ESPERANCE- MTU mmoja amefunguliwa mashtaka na maafisa wa
polisi nchini, baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja na kisha kunywa
shampeni na kulala kitandani.
Polisi wanadai
mwanaume huyo mwenye miaka 36, alivunja na kuingia katika nyumba hiyo mjini hapa,
Ijumaa ya wiki iliyopita.
Inadaiwa kuwa,
mtuhumiwa huyo alilewa baada ya kunywa kinywaji hicho. Mwenye nyumba alirudi
nyumbani na kumkuta mwizi huyo amelala kitandani mwake.
“Alitoka nje
na kuwapigia simu polisi, ambao walifika na kumkamata mtuhumiwa,” alisema Sajenti
Richard Moore.
Moore
alisema polisi walilazimika kumpeleka mtuhumiwa huyo hospitalini, baada ya
kukutwa amelewa chakari na atafunguliwa mashtaka ya wizi.
SHARE
No comments:
Post a Comment