Wayne Rooney ameiongoza klabu yake
mpya Everton kuishinda klabu ya Kenya ya Gor Mahia kwa kufunga bao zuri katika
mechi ya kirafiki iliyodhaminiwa na Kampuni ya Sportpesa.
Rooney aliiweka kifua mbele Everton kunako dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza ambacho Gor Mahia ilionekana kucheza vizuri kuwashinda wageni hao.
Hatahivyo Gor Mahia haikusubiri kwani baada ya mpira kuanzishwa katikati walipata kona iliopigwa na George Odhiambo ambapo ilimpata JacquesTuyisenge katika eneo zuri na hivyobasi kusawazisha kupitia kichwa kikali ambacho kipa wa Everton alishindwa kuokoa.
Kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza timu hizo zilikuwa na sare ya 1-1. Timu zote mbili zilifanya mabadiliko huku Rooney akitolewa baada ya kipindi cha kwanza.
Bao la Rooney lilirudisha kumbukumbu za bao lake dhidi ya Arsenal akiichezea Everton.
Katika kipindi cha pili Everton ilionekana kuimarika zaidi huku ikitishia lango la Gor Mahia mara kwa mara.
Na ilipofika dakika ya 81 kipindi cha lala salama Everton ilijiweka kifua mbele kupitia kiungo wa kati Kieran Dowell aliyewageuza mabeki wa Gor Mahia na kucheka na wavu.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment