Utata umegubika mdahalo wa moja kwa moja ambao unafaa kuwashirikisha wagombea wenza wa urais nchini Kenya.
Maandalizi ya mdahalo huo yanaendelea katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA).
Katika awamu ya kwanza, ni mgombea mmoja pekee aliyejitokeza, Eliud Muthiora Kariara ambaye ni mgombea mwenza wa Japheth Kaluyu.
Baadhi ya wagombea wenza wa urais walikuwa wametangaza kwamba hawatashiriki katika mdahalo huo ambao ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA).
Hatua ya wagombea kutojitokeza imeonekana kuwakera baadhi ya Wakenya mtandaoni, mfano Edwin Bakanja aliyeandika: "Ukikosa kufika kwa mahojiano, usisubiri upewe kazi."
SHARE









No comments:
Post a Comment