Kampuni ya
Moovn Technologies kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC, wamezindua
ushirikiano mpya utakaowarahisishia wateja wao kupata huduma ya usafiri
na kuwafikishia
huduma za simu watu zaidi ya milioni 12 barani Afrika.
Moovn
ni teknalojia inayomwezesha mtu anayetaka usafiri kuupata kwa haraka
akiwa sehemu alipo kwa kutumia
simu yake ya mkononi au kompyuta. Teknalojia hii pia inawawezesha watu
kufikishiwa bidhaa kutoka sehemu mbali mbali na madereva.
Ushirikiano huu kati ya Vodacom ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa ya simu za mkononi Afrika pamoja
na Moovn, utawawezesha watu zaidi ya milioni 12 kujiunga kwenye huduma hiyo ya Moovn app kwa kupitia simu zao za mkononi.
Kupitia mpango huo, kampuni ya Vodacom itatoa bure au kwa punguzo huduma za data kwa wateja wa Moovn pamoja
na madereva ili waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.
Wateja
wa huduma hiyo wataweza kuchagua usafiri wa aina mbali mbali kama vile
boda boda, bajaji pamoja na
taxi kulingana na mahitaji yao kwa kutumia Moovn app. Pamoja na kulipa
kwa fedha taslimu, wataweza pia kulipa kwa kutumia huduma ya kifedha ya
M-Pesa
Huduma
hii ya aina yake inalenga kuboresha maisha ya wateja wa kampuni zote
mbili zilizo kwenye ushirikiano.
Ushirikiano huu pia unalenga kutengeneza ajira pamoja na kuboresha hali
ya kiuchumi kwa jamii za Kitanzania na Afrika kwa ujumla.
“Tunayo furaha kuungana na mshirika mwenzetu katika kutoa huduma hii muhimu tukilenga kwa pamoja kubadili
maisha ya watu,” anasema Godwin Gabriel ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Moovn
Kumhakikisha
mteja usalama wake, mtumiaji wa huduma hii anaweza kubonyeza batani
inyoitwa ‘panic button’
na ujumbe mfupi wa maandishi utatumwa kwa mtu wake wa karibu ukieleza
sehemu alipo na utambulisho wa dereva muda wowote wakati akiwa kwenye
chombo cha usafiri.
Kipengele
hiki cha usalama ni muhimu kwa kuwa kwa siku za hivi karibuni kumekuwa
na matukio ya abiria kufanyiwa
uhalifu na baadhi ya madereva wasio waaminifu. Mteja pia anaweza
kuwafamisha ndugu jamaa na marafiki zake kinachoendelea kuanzia mwanzo
hadi mwisho wa safari yake.
Pamoja na mambo mengine, huduma hii itawawezesha wafanyabiashara kufuatilia bidhaa na huduma wanazowapelekea
wateja wao kuanzia wanapomkabidhi dereva hadi zinapomfikia mteja.
Madereva watakuwa wakipata malipo yasiyobadilika (Flat commission) kwa kila safari watakokuwa wakifanya
na kwa upande wao wateja watafurahia gharama zisizopanda.
Naye
Mkurugenzi wa kitengo cha biashara wa Vodacom Hisham Hendi alisema
“M-Pesa inawawezesha watu wote kuweza
kufikiwa na huduma ya kifedha kwa urahisi katika sehemu walipo.
Wakati
tukifanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanafikiwa na
huduma za gharama nafuu za kifedha, tunaendelea pia kuwaletea wateja
wetu huduma zenye ubunifu zinawezesha Serikali
na biashara kuwasiliana huku tukitoa malipo mazuri kwa mawakala wetu,”
Aliwashauri
watumiaji wa mtandao huo kwa kufanya malipo kwa njia ya simu kwani ni
salama zaidi kuliko kubeba
fedha taslimu. Kupitia huduma ya LIPA KWA M-PESA alisema malipo katika
huduma nyingi na bidhaa yamerahisihwa kupitia App mpya ya M-Pesa
SHARE
No comments:
Post a Comment