Mtayarishaji
wa muziki Elly da Bway ambaye amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Rama
Dee amefunguka baada ya msanii wake kumaliza ugomvi wake na kituo cha
Clouds.
Akiongea
na Bongo5, producer huyo amesema kuwa kitendo hicho kimemfurahisha na
kimeleta amani kwake kutokana na kukosa dili la kufanya kazi na wasanii
wengine kutokana na ugomvi huo.
Watu
wengi walikuwa hawaelewi hii ishu ilivyotokea, walikuwa wakisikia
nafanya kazi na Rama Dee moja kwa moja bila hata kufatilia kitu chochote
wanakuwa wananijumuisha mimi kwenye mgogoro huo pamoja na studio yangu
ninayofanyia kazi. Niliumia sana kwa kuwa hilo liliwafanya wasanii wengi
wawe waoga kuja kufanya kazi katika studio zetu mpaka ikafika wakati
nikaanza kumshawishi Rama aweze kuweka mambo sawa ilimradi tu niweze
kufanya kazi na kila msanii,” amesema Elly.
“Napenda
kuwa shukuru Clouds pamoja na maneno yote yaliowahiu kuongelewa lakini
walisupport kazi zangu zote nilizotengeneza na hata wimbo wangu mpya wa
‘Boss’ ambao nimeuachia mwezi uliopita umekuwa ukipewa nafasi kubwa
kwenye kituo hicho na vituo vingine tofauti tofauti hapa nchini,”
ameongeza.
SHARE
No comments:
Post a Comment