Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA) Joseph Kihanda, akitoa nasaha zake kwenye hafla
ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi hiyo. Uzinduzi huo
umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza muda mfupi kabla hajazindua Bodi
mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo
umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri
ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Said Chiguma akizungumza kwenye
hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya
TIA tawi la Singida mjini.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Ashatu Kijaji, akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi
mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo
umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA Singida mjini. Kushoto
kwake ni Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri TIA Said Chiguma na Afisa
Mtendaji Mkuu wa TIA Joseph Kihanda na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya
Singida Mhe. Elias Tarimo na Mjumbe wa Bodi Dkt. Leonada.
……………………
NA: MWANDISHI WETU
SINGIDA
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amezindua Bodi mpya
ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa lengo la kuimarisha
ufanisi wa Taasisi na uangalizi wa karibu.
Akizungumza
hivi karibuni wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Taasisi ya Uhasibu
Tanzania kampasi ya Singida Dkt. Kijaji amesema Bodi hiyo itamsaidia
Waziri wa Fedha na Mipango kupata ushauri wa kitaalam na hatimaye kutoa
maamuzi yenye tija kwa Taasisi na Taifa kwa ujumla.
“Bodi
hii ya Ushauri inategemewa kutoa mchango wa mawazo na kitaalam
yanayohusu uendeshaji na uboreshaji wa Taasisi yetu ya TIA ili
kuendana na mabadiliko yanayoendelea duniani katika nyanja mbalimbali za
kiuchumi, kiteknolojia, kisiasa na kijamii”, amesema Dkt. Kijaji.
Dkt.
Kijaji ameongeza kuwa Bodi hiyo ina wajibu wa kujua ubora wa wanafunzi
wanaohitimu katika chuo hicho ikiwa ni pamoja na ubora wa vyeti vyao
kuendana na uwezo wao wa kufanya kazi katika fani walizosomea na
kukabiliana na changamoto kwenye maeneo ya kazi.
Nae
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Said
Chiguma amesema Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchache wa
miundombinu kama vile kumbi za mihadhala, madarasa, maktaba na maabara
za kompyuta ambavyo ni nyenzo muhimu katika utoaji wa elimu iliyo bora.
Chiguma
amesema ili kupunguza changamoto hizo, Taasisi inajitahidi kutenga
fedha inazozikusanya ili kukarabati na kujenga majengo mbalimbali kwa
ajili ya kuboresha elimu na kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi
zaidi.
Taasisi
ya Uhasibu Tanzania ni chuo cha Serikali ambacho kinatoa mafunzo katika
fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa
Rasilimali Watu, Masoko na Uhusiano wa Umma pamoja na Uhasibu wa Fedha
za Umma kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashada (Diploma)
na Shahada (Degree).
SHARE
No comments:
Post a Comment