.
Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza John Mongella (katikati), akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi baada ya kuzindua Klabu ya Biashara
mjini Mwanza hivi karibuni. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim
Hussein. NBC imezindua Klabu ya Biashara iliyopewa jina la ‘NBC B-Club’ katika
miji ya Kahama na Mwanza kwa kuandaa semina kwa wafanyabishara wajasiriamali. NBC B-Club itasaida huduma zisizo za kifedha kupitia mafunzo
maalumu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
kuhusu mbinu za uendeshaji wa biashara na kuwajengea uwezo katika kuziendesha
kwa ufanisi hivyo kukuza biashara hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi
akihutubia wakati sherehe za uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara jijini Mwanza
hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim
Hussein, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliyekuwa mgeni rasmi na
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.
Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, John Mongella akihutubia wakati wa semina ya wafanyabiashara
katika uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC mjini Mwanza. Wengine kutoka
kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa NBC, Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Filbert
Mponzi.
Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati), akizungumza na ujumbe wa viongozi wa
NBC waliofika ofisi kwake kumtembelea wakiongozwa na Dk. Kassim Hussein (kulia
kwake) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theoblad Sabi (kushoto kwake). NBC
ilizindua klabu za biashara katika miji ya Kahama na Mwanza pamoja na
kusherehekea miaka 50 tangu ilipoanzishwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika sherehe za
maadhimisho ya mika 50 ya benki hiyo mjini Mwanza.
Mjumbe
wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein (mwenye tai nyekundu), Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji, Theobald Sabi na Mkuu wa
Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha pamoja na wateja na waalikwa wengine wakijipiga
picha maarufu kama ‘selfie’ kama moja ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka
50 ya NBC jijini Mwanza.
SHARE
No comments:
Post a Comment