Rais wa
Palestinia, Mahmoud Abbas amekata mawasiliano na serikali ya Israel
hivyo kuzidisha mzozo ambao umekuwa ukitokota wiki nzima kuhusu hatua
kali zaidi zilizochukuliwa na Israel huko mji wa kale wa Jerusalem.
Ghasia zilizuka pale polisi wa Israeli walipoweka vizuizi kuwazuia wanaume wote chini ya miaka 50 kushiriki salah ya Ijumaa katika msikiti wa Al-Aqsa eneo linalozozaniwa na pande hizo mbili kinzani.
Eneo hilo takatifu la ibada mjini Jerusalem, maarufu kama Hara al-Sharif, kwa waumini wa kislamu na Hekalu la mlimani kwa wayahudi.
Ripoti zaongeza kusema kuwa raia watatu wa Israel pia waliuawa katika mzozo huo huko eneo la ukingo mwa magharibi - West Bank
SHARE
No comments:
Post a Comment