*TAARIFA
MUHIMU KWA WAGOMBEA WA UVCCM KATIKA DHAMIRA YA KUJENGA HAIBA YA
DEMOKRASIA YA KWELI NA KURUDISHA UPYA MAADILI NA NIDHAMU YA UCHAGUZI
HURU*
Demokrasia
ni jambo muhimu linalohitajika kuheshimiwa na kuenziwa ndani na nje ya
Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa miaka kadhaa kumekuwa na
shutuma pia tuhuma zilizokaribia kuotesha mizizi ya kuwepo rushwa
ambazo nusra zivunje heshima ya chama chetu na jumuiya zake. Jambo hilo
sasa halitaruhusiwa tena wala kuachiwa lifanyike .
Kiongozi
wa UVCCM mahali popote atachaguliwa baada ya kufanyika chaguzi huru na
za haki, kuzingatia Kanuni na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoagizwa na
vikao husika bila ya kukiuka, kupuuzwa au kuvunjwa.
Nia
ya UVCCM ni kujenga haiba mpya na njema ya kuheshimu misingi ya
demokraia ya kweli, kuwa na adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili
kwa kila anayetaka kuchagua au kuchaguliwa.
Jana
Jumapili tarehe 02/07/2017 zoezi la utoaji fomu kwa Waombaji wa nafasi
mbali mbali za Uongozi katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM lilianza
rasmi ngazi ya Wilaya, Mikoa na Taifa.
•
Kwa Ngazi ya Taifa nafasi zote fomu zinatolewa Dodoma ghorofa ya 3
chumba Na. 45, Ofisi Ndogo za UVCCM Dar es Salaam ghorofa ya 7 na Afisi
Kuu ya UVCCM Gymkana Zanzibar.
Fomu zote zirejeshwe si zaidi ya tarehe 10/07/2017 Saa 10.00 Jioni katika maeneo yaliyoainishwa.
Ifahamike
kuwa kila Kijana wa Chama Cha Mapinduzi ana haki ya msingi kugombea
nafasi yoyote ile kwa mujibu wa Kanuni ya UVCCM na katiba ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
•Kama
iliyo Haki na Wajibu wa mwanachama kugombea, kuchagua au kuchaguliwa,
ndivyo inayostahili mwanachama kufuata taratibu na kuheshimu kanuni
pamoja na taratibu za uchaguzi.
•UVCCM
imekusudia kurudisha nidhamu ya Chama hasa katika suala zima la
kugombea nafasi za uongozi na haki ya kuchagua au kuchaguliwa.
•Muomba
nafasi anayo haki ya kutia nia, kuchukua fomu ya kuwania Uongozi bila
ya kufanya mbwembwe, shengesha au mikogo ambayo kwa namna moja au
nyingine itaonyesha hali ya kujinadi mapema, kujitangaza na kufanya
kampeni.
•
Muomba nafasi yoyote ajaze fomu zake kwa uangalifu, azingatie tarehe
na siku ya kurudisha mahali husika tena kwa kujali wakati uliopangwa
kikanuni na kuheshimu taratibu.
•Sifa
au wasifu wa kila muomba nafasi kwa kadri atakavyojaza fomu yake
utajielekeza na kuandikwa kama ilivyo katika kitabu maalum cha wagombea
wote ambacho kitasomwa na wajumbe wapiga kura siku ya uchaguzi husika
hivyo ni vyema kuwa makini na taarifa zako.
•Ni
marufuku na hatakiwi kabisa muomba nafasi yoyote ile Mara baada
kuchukua au kurejesha fomu kuandika bango au kipepeprushi na kuvigawa,
kuvieneza au kuwatuma wapambe wake wakati taratibu nyengine za vikao
bado hazijakamilika.
*Kila
muomba nafasi atapata nafasi ya kujieleza, kutoa wasifu wake, kutaja
dhamira na malengo yake mbele ya wajumbe wa Mkutano husika wa
kuchaguliwa si kinyume na hivyo baada ya taratibu za Vikao kukamilika.
•Kuanza
mapema kampeni au wapambe kufanya ushabiki wa kisiasa na kumnadi,
kumpiiga debe pia kwenda katika vyombo vya habari na kueleza wasifu,
sifa au kutaja nafasi anayogombea na kujinadi kutahesabika ni kufanya
kampeni mapema na kumfanya apoteze sifa.
•Ni
marufuku na haitaruhusiwa kabisa muda ukifika kwa mgombea yeyote
kufanya kampeni za kihuni kwa kutumia lugha chafu, siasa za maji taka,
matusi, dharau kinyume na ubinadamu pia kushiriki kejeli dhidi ya
wenzake.
•Muomba
nafasi katika ngazi yeyote ambaye hatazingatia wala kuheshimu na
kutofuata maelekezo haya anaweza kujipotezea sifa ya kuteuliwa na
kushiriki kwake katika chaguzi huru na za kidemokrasia ndani ya UVCCM
*ANGALIZO:*
•
Kuachia hayo yote yafanyike bila ya kuyadhibiti , kuyaasa na kuyakemea
ni mwanzo wa kuiruhusu au kufungua milango atakayopita adui rushwa .
•Rushwa
ni kikwazo cha maendeleo ya demokrasia na adui hatari wa haki,
haitakubalika wala kuruhusiwa muomba nafasi kutoa au kupokea na kugawa
rushwa ndani ya chaguzi za jumuiya yetu.
•Chaguzi
za jumuiya zitafanyika kwa njia huru na za uwazi huku kila na mgombea
akipitishwa jina lake na vikao husika vya Kikanuni na Kikatiba baada ya
kuonekana kuwa amekidhi masharti na kufuata kanuni za uchaguzi katika
kila hatua husika bila kukiuka.
•Uchaguzi
ni kipimo cha ukomavu wa demokrasia ya kweli bila kufanyika mizengwe na
hila ndani ya jumuiya kwa lengo la kusimamia shabaha na misingi sahihi
itokanayo na miongozo, maelekezo na kuheshimu utaratibu unaohimizwa na
Chama Cha Mapinduzi na kutii maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na
Mwenyekiti wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli.
•Waomba
nafasi hawaruhusiwa kutembea toka Wilaya au Mkoa mmoja hadi mwingine,
kukusanya wajumbe, kujinadi au kuelezea dhamira yake ya kuchukua fomu
kabla ya siku ya uchaguzi kwani kuyaachia hayo na mengine yafanyike huko
ni kuipalilia rushwa istawi ndani ya chaguzi zetu .
Ni
matumaini yangu kuwa Vijana mtaendelea kujitokeza kwa wingi kuchukua
fomu za kuomba Uongozi kutimiza haki yenu ya Kidemokrasia ndani ya
Jumuiya yetu.
Nawatakia kila la heri.
*KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI*
*Shaka Hamdu Shaka* *(MNEC)*
*KAIMU KATIBU MKUU*
SHARE
No comments:
Post a Comment