Wanajeshi wa Mali
BAMAKO, MALI
WANAJESHI takriban 10 wa Mali wamepoteana baada ya kufanyiwa kushambuliwa na wapiganaji wa itikadi kali, Jeshi la nchi hiyo limesema.
Walishambuliwa wakiwa katikati ya miji ya Gao na Menako siku ya Jumapili, alisema Msemaji wa jeshi, Kanali Diarran Kone. Inadaiwa kuwa wapiganaji hao wana uhusiano na mtandao wa al Qaeda.
"Tumevamiwa, wanajeshi wetu takriban wamepotezana na magari yetu manne yamepotea. Tunafanya tathmini halisi ya tukio hili," alisema Kone.
Wapiganaji hao wanashikilia eneo kubwa kaskazini mwa Mali tangu mwaka 2012. Jitihada zinazofanywa na majeshi yanayoongozwa na Ufaransa bado hazijazaa matunda kukabiliana na wapiganaji hao ambao hufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Hata hivyo, hali ya usalama inatia matumaini tofauti na siku za nyuma.
SHARE
No comments:
Post a Comment