TRA

TRA

Friday, July 14, 2017

Simba apatikana akimnyonyesha mwana wa chui Tanzania

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




Simba apatikana akimnyonyesha mwana wa Chui Tanzania



Mwana wa chui hawezi kubadili madoa doa katika ngozi yake lakini simba huyo hajali hilo.

Picha hizi ni za kwanza kuchukuliwa simba akimnyonyesha mwana wa chui kutoka jamii nyengine ya wanayama, kisa kisicho cha kawaida.

Wawili hao walionekana na Joop Van Der Linde mgeni katika katika eneo la Ndutu safari Lodge nchini Tanzania katika eneo la uhifadhi la wanyama pori la Ngorongoro. 

Eneo hilo ni la Serengeti. Simba huyo amepewa jina Nosikitok na ana umri wa miaka mitano.

Simba huyo amewekewa mfumo wa GPS katika shingo yake ili kutambua anakokwenda na ana watoto watatu waliozaliwa kati ya mwezi Juni 27-28. 

Daktari Luke Hunter , ambaye ni rais mhifadhi mkuu wa Panthera ,shirika kuu la ufugaji wa wanyama aina ya paka aliambia BBC kwamba kisa hicho ni cha kipekee. 

Sio kitu ambacho nilijuwa ambapo simba angeweza kuwalea watoto wa simba mwengine.,...hiki ni kisa tofauti sana.

Sina kisa chengine chochote nikijuacho kati ya familia ya mnyama paka kwa mfano pale ambapo mnyama mmoja amechukua mwana wa mnyama mwengine katika familia hiyo hiyo na kumnyonyesha.

Simba wengi wa kike huwauwa watoto wa chui wanapokutana nao, na huwaona kama wapinzani katika mapambano ya kutafuta chakula.

Daktari Hunter anasema Nosikitok ana watoto wachanga walio na umri sawa na mwana huyo wa chui wakiwa na wiki mbili hadi tatu hivi. nyumba yao ambapo kuna maficho ya watoto wake alipokutana na chuo huyo mdogo.

Alimchukua mwana huyo na kumlea kama wake na humlindi dhidi ya shambulio lolote.a

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger