………………………………………………………
Kampuni
ya simu za mkononi ya Tigo, ambayo ni kinara wa ubunifu wa mitindo ya
maisha ya kidijitali nchini, imetangaza mageuzi katika uwekezaji ili kuboresha upatikanaji wa mtandao ili kuweza kuwapatia huduma bora zaidi wateja wake wa matumizi ya sauti na data.
Akizungumza
na wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini, Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Ufundi na mawasiliano wa Tigo, Jerome Albou,amesema kampuni hiyo imewekeza kiasi cha dola za kimarekani millioni 75 kwenye mradi mkubwa wa kuendeleza mtandao huo.
Alisema
moja ya malengo yao kimkakati ni kubadilisha uzoefu wa wateja kwa
kuwapatia mtandao wenye ufanisi kulingana na viwango vya sekta ya
mawasiliano ambapo katika miaka mitatu iliyopita Tigo imeweza kuongeza
msingi wa wateja wake kufikia zaidi ya milioni 10.
“Kadri tunavyoendelea kukua, kupanua mtandao
na kuufanya kuwa wa kisasa zaidi, ni jambo la lazima kutoa huduma bora
zaidi,” alisema Albou huku akiongeza kwamba kuanzia mwaka jana kampuni
ya Tigo imefanya upanuzi mkubwa wa miundo mbinu ili kuweza kufikia
maeneo mengi nchini .
“Mahitaji
ya matumizi ya data yamekuwa yakiongezeka kila siku, hivyo Tigo imeweza
kuhakikisha matumizi ya 3G na 4G yanaweza kuwafikia watumiaji
vijijini,” aliongeza Albou
SHARE









No comments:
Post a Comment