

BENKI ya NMB imesisitiza kuwa
huduma ya ‘Trade Fainance’ inayotolewa na benki hiyo inatarajiwa
kuchochea ukuaji wa biashara ndani na nje ya nchi kwa Wafanyabiashara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye
semina, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker alisema
huduma hiyo imewalenga wateja muhimu katika makundi yote ya
wafanyabiashara wa kati na wakubwa ili kuzikuza biashara zao.
Alisema huduma ya ‘Trade Finance’
ni muhimu kwa biashara za ndani ya nchi na kimataifa, na Benki ya NMB
imeiweka kuhakikisha inasaidia kukuza biashara zao. “Kwa lengo la
Serikali ya Awamu ya Tano, kujenga uchumi wa viwanda kuna kila sababu ya
Benki kubwa kama NMB kusaidia kukuza masoko kupitia huduma yake ya
‘Trade Finance’,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Bussemaker
alipokuwa akifungua semina hiyo kwa wanahabari.
Aidha alifafanua kuwa, lengo la
kampeni ya huduma ya NMB Trade Finance ni kuhakikisha inaonesha uhimara
na ubora wa huduma yenyewe kibiashara na kuitangaza kwa wafanyabiashara,
huku ikibainisha ilivyo msaada kwa bidhaa na huduma mbalimbali za
wafanyabiashara ndani na nje ya nchi.




SHARE








No comments:
Post a Comment