WANAFUNZI wanaosoma shule ya sekondari ya Kwamkabara kata ya Kwamkabara wilayani Muheza mkoani Tanga wamepatwa na ugonjwa wa ajabu unaosababisha kuanguka ovyo.
Ugonjwa huo umesababisha wanafunzi 52 mpaka 70 wanaanguka baada ya kushikwa na ugonjwa waajabu wa kuanguka na kupiga kelele pamoja na kutokwa ute mdomoni kama wamepandisha mashetani.
Tukio hilo limetokea juzi katika shule hiyo ya sekondari ya kata ya Kwamkabara wilayani Muheza mkoani Tanga. Mkuu wa shule hiyo Getrude Moyo amethibitisha kuwapo tukio hilo la watoto kuanguka na kupiga kelele.Akizungumza eneo la tukio Ofisa elimu wa shule za msingi wilayani Muheza, Julitha Akko amesema kuwa wanafunzi hao walishikwa na ugonjwa wa kuanguka na kupiga kelele kama wamepandisha mashetani.
Akko alisema kuwa mpaka sasa chanzo cha wanafunzi hao kuanguka na kupiga kelele bado hakijafahamika na wazazi kwa kushirikiana na walimu wa shule hiyo walifanya maombi ya kukemea mapepo katika shule hiyo na baadae wanafunzi hao kuchukuliwa na kurudi nyumbani.
SHARE
No comments:
Post a Comment