TRA

TRA

Monday, July 10, 2017

Upinzani Zimbabwe wamtaka Mugabe ajiuzulu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao


Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimerejelea wito wao wa kutaka Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 ajiuzulu, na kumlaumu kwa kuiongoza nchi kutoka hospitalini kufuatia madai kuwa alisafiri kwenda Singapore kwa matibabu.

Gazeti la kibinafsi la News Zimbabwe lilimnukuu Obart Gutu, msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha MDC akisema.
"yeye bado si kijana mdogo, njia hii anajiadhibu si nzuri kwa afya yake ya kimwili na kiakili.
Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe kusonga mbele chini ya uongozi mpya."
Karauone Chihwayi, msemaji wa upande uliojitoa MDC naye alitoa matamshi kama hayo.
"Nchi hii imekwama leo hii kwa sababu rais wa Zanu anaongoza akiwa kitanda cha hospitali."
Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao licha ya kuonekana kutokuwa na afya nzuri na amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger