TRA

TRA

Sunday, July 9, 2017

USIKUBALI KUPITWA, NENDA KAMUONE ROONEY UWANJA WA TAIFA JULAI 13

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

  Good news kwa mashabiki wa soka la Bongo ni kutoka jiji la Liverpool ambapo ndio makao makuu ya club ya Everton tunayoitarajia kuiona uwanja wa Taifa Dar es Salaam July 13 katika mchezo dhidi ya Bingwa wa SportPesa Super Cup Gor Mahia ya Kenya.

Wakati baadhi ya mashabiki wa soka bongo wakiwa wanasononekana kwa kukosa kumuona Romelu Lukaku akiwa na Everton kutokana na kukaribia kuihama timu hiyo, Everton wamethibisha kumsajili nahodha wa ManUnited Wayne Rooney.

Rooney amesaini Everton mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru akitokea Man United ambayo amedumu nayo kwa miaka 13 baada ya kuondoka Everton mwaka 2004, kutokana na Rooney kujiunga na Everton tutarajie kumuona Taifa katika mchezo wa maandalizi ya msimu dhidi ya Gor Mahia.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger