Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki
(Mb) katika Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam leo
Julai 18, 2017.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni,
ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Chama cha TALGWU, Ibrahim Zambi akiwasilisha hoja mbalimbali
zinazowahusu watumishi wa umma wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki
(Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika
leo Jijini Dar es Salaam.
Askari
Msaidizi wa Manispaa ya Ubungo, Bw. Germini Massawe akiwasilisha malalamiko kuhusu kada yake wakati
wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi
wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi-Idara ya Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Loyce Lugoye akifafanua
jambo kuhusiana na masuala ya kiutumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment