Jumamosi,
Julai 15, 2017, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Atufigwege Kasesela
alitembelea kituo cha kulea watoto wenye ulemavu kiitwacho Nyumba Ali
kilichopo Wilolesi. Nyumba Ali iliundwa na umoja wa wazazi wenye watoto
waishio na ulemavu mkoani Iringa.
Lengo
la kuunda umoja huo ulikuwa ni kuwakutanisha wazazi ili waweze kuwa na
sauti moja katika kubainisha na kusaidiana katika kutatua changamoto
mbalimbali zinazo ikumba jamii ya watoto waishio na ulemavu. Akitoa
taarifa Mbele ya Mkuu wa wilaya mratibu wa kituo hicho, Adam Duma
alisema wamefungua vituo hivyo viwili kimoja kikiwa Wilolesi na kingine
Ngome.
Kituo
kimoja kinapokea watoto 35. Wamekuwa wanawafanyia mazoezi ya viungo
pamoja na kuwafundisha kazi za mikono mbalimbali watoto wenye ulemavu wa
viungo na akili.
Akizungumza
na wazazi na walezi wa kituo hicho, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard
Kasesela alisema “ Nasikitishwa na baadhi ya wazazi ambao wanajaliwa
kupata watoto wenye ulemavu na kuwatelekeza hili halikubaliki.
Kila
afisa tarafa afanye utafiti nyumba hadi nyumba kubaini kama kuna mtoto
mlemavu, Nachukia sana tabia ya baadhi ya wakina baba kukimbia watoto
wenye ulemavu na kuwachia wakina mama. Hebu wanaume tuache tabia ya
kukimbia watoto wenye ulemavu.” alisema. Pia aliwataka wakina baba
wajitokeze kufika kwenye kituo sio kuwachia wakina mama peke yao.
Kituo
cha Nyumba Ali kimekuwa kikiendeshwa kwa msaada wa wahisani mbalimbali
ambapo mahitaji makubwa ni pamoja na chakula, baiskeli za walemavu
pamoja na gharama za uendeshaji.
Katika
kituo hiki yupo mtoto aitwaye Zawadi ambaye amesomeshwa hadi kiwango
cha darasa la saba, Mtoto huyu hawezi kutumia mikono anatumia miguu kwa
shida akisaidiwa na kompyuta na amefanikiwa kuandika kitabu kinacho
elezea maisha yake.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Atufigwege Kasesela akizungumza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu kiitwacho Nyumba Ali kilichopo Wilolesi, Wilayani Iringa.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Richard Atufigwege Kasesela akifurani na watoto
wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu kiitwacho Nyumba
Ali kilichopo Wilolesi, Wilayani Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Atufigwege Kasesela akizungumza na baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu kiitwacho Nyumba Ali kilichopo Wilolesi, Wilayani Iringa.
SHARE
No comments:
Post a Comment