Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua risiti ya mmoja wa
mama aliyefika kwenye hospitali ya Wilaya ya Chato aliyekuwa amemleta
mtoto wake kupata matibabu.Mhe.Waziri alikua akijiridhisha kama mama
huyo amelipishwa fedha katika matibabu ya mtoto kwakuwa matibabu kwa
mtoto chini ya miaka mitato huduma hutolewa bila malipo
Waziri Ummy akikagua duka la dawa
lililopo kwenye hospitali hiyo (Duka la MSD) ambalo linasaidia
upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo pamoja na vituo vya afya
pamoja na zahanati za jirani.Kulia mwisho ni Mbunge wa Jimbo la Chato na
naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani
Waziri wa Afya akitoka kutembelea
Wodi ya Wazazi iliyopo kwenye Hospitali hiyo,kushoto ni Mganga Mkuu wa
Wilaya Dkt. Athanasi Ngambakub na katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na
madini Dkt.Medard Kalemani
Waziri Ummy wakijadiliana jambo
kwenye jengo jipya linalojengwa la upasuaji,ambapo Waziri ameagiza jengo
hilo likikamilika wawape kipaumbele akina mama wajawazito ili kuweza
kuokoa vifo vitokanavyo na uzazi
Katika wodi waliyolazwa watoto Waziri Ummy akimsalimia mmoja wa mtoto aliyelazwa hospitalini hapo
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akimsisitiza jambo Waziri wa Afya wakati
wa kuongea na watumishi wa hospitali hiyo,kushoto ni Mkuu wa Wilaya
Mhe.Shabani Ntalambe
Dkt.Kalemani akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo(hawapo pichani) mara baada ya kutembelea hospitali hiyo
Meneja wa Kanda ya Mwanza wa
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Victory Sungusia akijibu swali toka kwa Waziri
Ummy wakati wa kuongea na watumishi wa hospitali ya Wilaya ya Chato
Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(hayupo pichani)
Picha ya pamoja ya
Mawaziri,Viongozi wa Mkoa na Wilaya pamoja na baadhi ya watumishi wa
hospitali hiyo mara baada ya kumaliza ziara (Picha zote na Wizara ya Afya)
SHARE
No comments:
Post a Comment