Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza Mheshimiwa Asha-Rose Migiro alifanya ziara
ya kuwatemebelea Watanzania waishio katika mji wa Bimingham na
vitongoji vyake tarehe 28/8/2017.
Pamoja
na ziara hiyo, Mhe. Balozi Migiro alipata nafasi ya kushiriki katika
uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania waishio katika mji huo wa
Birmingham na Vitongoji vyake, ijulikanayo kama Watanzania wa Birmingham
na nchi nyeusi -(Tanzanian's in Birmingham and Black Country - WBBC).
Mhe.
Balozi aliwapongeza na kutoa wito kwa Watanzania hao kuwa na
kushirikiano wa karibu na Ofisi za Ubalozi kupitia Viongozi wao. Pia
alihimiza umuhimu wa Wana diaspora kuwa wamoja na kushirikiana bila
kubaguana.
Katika
Mkutano huo, kulifanyika hafla ndogo ya kuchangia Jumuiya hiyo pamoja
na chakula cha pamoja kwa kumshukuru Mhe.Balozi kwa kutenga muda wake na
kuwatembelea.
Sambamba
na hafla hiyo Mheshimiwa Balozi Asha-Rose Migiro pia alizindua rasmi
Jumuiya hiyo, na kukabidhiwa Katiba yao itakayo tumika kuendesha
shughuli za kila siku za Jumuiya hiyo.
Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi Migiro akiwahutubia
Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo kushoto kwake ni katibu wa
Jumuiya ya Watanzania waishio Birmingham na Black Country Dkt. Hassan
Khalfan Hamidu, anayefuatia ni Mbunge kutoka jimbo la Stafford wa chama
cha Conservative Jeremy John Lefroy na nyuma ya Balozi ni Mwambata wa
Uhamiaji Ubalozini Bw. Magnus Ulungi.
Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi akiwa na viongozi wa Jumuiya
ya Watanzania waishio Birmingham Mwenyekiti wa WBBC Bw. Renatus
Mgetta(Pili kulia), Katibu wa Baraza la Ushauri Brian M. Ngelangela.;
Kutoka kushoto mwa picha ni Katibu Mwenenzi Dr. Dr. Othman M., Katibu wa
Jumuiya Dr. Hassan Khalfan na Kiongozi wa Kamati ya Katiba, Uratibu na
Mwongozo Bw. Nelson Kampa.
Mbunge kutoka jimbo la Stafford wa chama cha Conservative Jeremy John Lefroy akihutubuia katika mkutano huo wa wanadispora.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi Migiro akijumuika na watanzania katika kucheza muziki
Balozi Asha-Rose Migiro akizungumza na Mwenyekiti wa British Tanzania Society (BTS) Prof. Andrew Coulson wakati wa mkutano huo.
Mheshimiwa Balozi, akijumuhika na Watanzania hao katika chakula cha pamoja
SHARE
No comments:
Post a Comment