Walimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya
sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi
la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha
tatu shuleni hapo.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama, January Lugangika amesema waalimu wa wanafunzi hao
wamekikuka maadili ya ualimu na kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku
akiongeza kuwa tabia hizo zinaleta kichefu chefu kwa jamii.
Aidha mwenyekiti huyo amedai kuwa ushahidi wa tukio hilo umethibitishwa
na Daktari ambaye aliwafanyia vipimo na kuthibitisha ni kweli kitendo
hicho kilifanyika
Kwa upande wa Afisa elimu wa sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato
amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike muda
yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao.
"Inabidi wazazi muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya
nini shuleni na kama mzazi humfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua
na badala yake ukashtukia ana mimba ya miezi hata sita," alisema
Singato.
SHARE
No comments:
Post a Comment