Wakicheza
bila ya mshambuliaji wao hatari Neymr amabye amehamia PSG pamoja na
Luis Suarez aliye na majeruhi timu ya Barcelona imeanza vyema katika
kusaka taji la Ligi Kuu ya Hispania kwa kupata ushindi wa magoli 2-0
katika mechi yake ya La Liga dhidi ya Real Betis.
Wakicheza
kwa kujiamini licha ya kufungwa na mahasimu wao wakubwa Real Madrid
katika mchezo wa Ngao ya Hisani walipata magoli yao kupitia kwa Alin
Tosco aliyejifunga dakika ya 36 huku beki Sergio Roberto akipingilia
msumari wa pili dakika ya 39.
Kipindi
cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko
hayo hayakuweza kuwasaidia Real Betis hadi dakika 90 Barcelona
wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0 na pointi tatu muhimu.
Katika
Uwanja wa Camp Nou, kulikuwa na ulinzi wa ziada kutokana na shambulio la
kigaidi lililotokea siku tatu zilizopita na kusababisha vifo vya watu
14.
SHARE















No comments:
Post a Comment