
Taarifa
iliyonifikia usiku huu kutoka Tarime mkoani Mara ni kuwa Mbunge wa Bunda
Mjini Ester Bulaya amewahishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime
baada ya kuugua akiwa rumande ambako alikuwa ameshikiliwa na Polisi
baada ya kumkamata akiwa Hotelini, Tarime.
Katibu wa
Mbunge Tarime Vijijini, John Heche, Mrimi Zabron amesema Bulaya
anasumbuliwa na kifua ambacho kimesababisha ashindwe kuzungumza lakini
hata hivyo Madaktari wanaendelea na matibabu.
SHARE








No comments:
Post a Comment