....................................................................................................................................
Na Ezekiel Kamanga ,Matukiodaima Mbeya
ABIRIA zaidi ya 50 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya kampuni ya Saibaba aina ya Scania lenye namba za usajili T 131 AZZ likitokea Dar es Salam kwenda Sumbawanga kuacha njia na kupinduka eneo la Chimala wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 1:20 usiku Agosti 27 mwaka huu kuwa basi lilikuwa linaendeshwa na dereva Hussein Mkwizu(52)mkazi wa jijini Dar es Salaam na kusababisha majeruhi watano ambao wamelazwa Hospitali ya Chimala.
Mpinga amesema chanzo cha ajali ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa basi alipojaribu kulipita lori ndipo basi lilipoteza mwelekeo na kupinduka.
Ametoa wito kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani na Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa madereva wazembe.
SHARE
No comments:
Post a Comment