Mwenyekiti
wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege
(kushoto) akiongea na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo
ulioambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kulia).
Benki ya Kilimo ilifanya ya ukaguzi wa miradi iliyopatiwa mikopo ili
kujionea maendeleo ya miradi wilayani Kilombero.

Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza
wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyokopeshwa na Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wilayani humo. Wengine pichani ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na
viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo.

Makamu
Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Bw. Mohamed Dadi (kushoto)
akionesha maendeleo ya Skimu hiyo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilombero
Bw. James Ihunyo (wapili kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka
wilayani na Benki ya Kilimo walipotembelea Skimu hiyo.

Kaimu
Afisa Tarafa ya Mang’ula, Bw. Omary Said (kulia) akitoa maelezo kuhusu
Mradi wa Kilimo Shadidi kinachofanyika katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa
kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (kushoto) na Umoja wa
Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw.
Francis Assenga (katikati). Wengine wanaosikiliza na viongozi
waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo

Meneja
Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Bw. Dickson Pangamwawe
(wapili kushoto) akionesha maendeleo ya ukuaji wa miwa ya Umoja wa
Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa ambao ni wanufaika wa mikopo ya Benki
ya Kilimo. Wanaotazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili
kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa
Ujamaa, Bw. Sebastian Sanindege.

Maafisa
kutoka Benki ya Kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero
wakingalia Mpunga uliyo tayari kuvunwa katika Skimu ya Umwagiliaji ya
Kijiji cha Msolwa Ujamaa.

Wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kijiji cha Msolwa Ujamaa wakipanda mpunga kwa kutumia njia ya kilimo shadidi.
………………………………………………………………
Katika
kuhakikisha miradi inayopatiwa mikopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB), uongozi wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Mkuu wa
Wilaya ya Kilombero, Bw. James Ihunyo wametembelea miradi minne iliyopo wilayani humo.
Miradi
iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula. Nyingine
ni Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga alisema ameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo hali
inayochochea ari ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha
wakulima nchini.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo aliwaasa wakulima hao kurudisha mikopo kwa wakati ili wakulima wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.
“Lengo
la mikopo hiyo ni kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini
Tanzania, hivyo kuchelewesha mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma
juhudi hizi,” Bw. Ihunyo alisema.
Zaidi ya Shilingi bilioni 2 imekopeshwa kwa wakulima wa mpunga na miwa wilayani Kilombero
SHARE








No comments:
Post a Comment