
Ndugu zangu,
Miaka
hiyo tuko Primary na Sekondari tulikuwa tukiwasoma waandishi mahiri na
wengine wenye majina ya kutisha, ni wakongwe aina ya Ndimara Tegambwage,
John Rutayisingwa, Stanley Kamana na wengineo.
Kwenye
maktaba yangu ninaye mkongwe Ndimara Tegambwage. Huyu kila tukikutana
lazima tubishane kwa hoja. Napenda kumchokoza ili nipate kuchimba madini
yaliyo kichwani mwake.
Moja
ya kumbukumbu zangu ni usiku ule pale Kinondoni zilipokuwa ofisi za
gazeti la Mwanahalisi. Nilifika mahali hapo kama saa moja usiku.
Nilikuwa na kawaida ya kufika hapo kukutana na kusalimiana na ndugu
zangu kwenye habari.
Pale chumba cha habari niliwakuta ndugu yangu Saed Kubenea, Jabir Idrissa na Mwalimu na Mzee wangu Ndimara Tegambwage.
Haikuchukua muda tukaanza kubishana kwa hoja mimi na Ndimara juu ya hoja ya kama gazeti lina jukumu ya kuandika yaliyo mazuri pia ya Serikali au chochote kizuri kinachofanywa na Serikali ni wajibu wake na haina haja ya kusifiwa. Tulibishana sana na nikavuna mengi kutoka kwa Mwalimu wangu Ndimara.
Haikuchukua muda tukaanza kubishana kwa hoja mimi na Ndimara juu ya hoja ya kama gazeti lina jukumu ya kuandika yaliyo mazuri pia ya Serikali au chochote kizuri kinachofanywa na Serikali ni wajibu wake na haina haja ya kusifiwa. Tulibishana sana na nikavuna mengi kutoka kwa Mwalimu wangu Ndimara.
Siku
mbili baadae, mahali hapo hapo katika muda kama huo, kukatokea tukio la
kusikitisha la Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage kushambuliwa na
wasiojulikana na hata Kubenea kujeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa tindikali
machoni.
Binafsi
nimemsoma Mwalimu wangu Ndimara tangu nikiwa Sekondari pale Tambaza. Si
wengi wenye kujua, kuwa Ndimara alipata kuwa mwandishi wa magazeti ya
Chama, Uhuru na Mzalendo.
Si wengi pia wenye kujua, kuwa Ndimara aliasisi gazeti lake lililoitwa 'Radi'.
Na si wengi wenye kujua kuwa Ndimara alipata kuwa Mweka Hazina wa NCCR Mageuzi na hata akawa mbunge kwa muhula mmoja.
Mwalimu wangu Ndimara anazijua harakati za siasa za upinzani, na anaifahamu vema media ya nchi hii.
Tukibaki
kwa Ndimara kama Mwanahabari, hakika, enzi hizo Radi ilikuwa radi kweli
kweli. Ilishuka mara moja kwa mwezi. Ilipopiga Radi ya Tegambwage hata
Ikulu ilitikisika.
Nakumbuka toleo namba moja la Radi lilikuwa na habari kuu yenye kichwa cha habari mithili ya radi;
"Kutawaliwa Kama Kondoo Sasa Basi..!" Hiyo ilikuwa radi haswa iliyoshuka Ikulu ya Mzee Mwinyi!
Nina
mengi ya kusimulia ya wakati huo tukisoma magazeti aina ya Radi, Moto
Moto, Family Mirror, Fahari, Michapo, Wasaa, Mshindi, Mizani hadi Sauti
Ya Siti!
Maggid,
Iringa.
Iringa.
SHARE
No comments:
Post a Comment