Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb), (kulia) akipata ufafanuzi wa Utaratibu wa malipo ya kiinua mgongo,
pensheni na mirathi alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango. Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Mipango Bi. Joyce Mkinga
pamoja na Mkuu wa Hazina Ndogo Lindi, Pili Kamali.
NA WFM,
LINDI
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) amewataka watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi
zake kuwahudumia wananchi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa wananchi na
Serikali yao.
Dkt Mpango aliyasema hayo alipotembelea banda la
Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya maonesho Nanenane katika eneo la
Ngongo mkoani Lindi.
Alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inategemewa na
wananchi wengi hivyo ni vyema wahudumiwe vizuripamoja na kutoa elimu kwa umma
vya kutosha ili waweze kuelewa na kuridhika na huduma zinazotolewa na wizara.
“Tujitahidi kuwaelezea wananchi juu ya kazi na huduma
zetu ili waweze kuzitumia kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla na tuweze kufikia
uchumi wa viwanda kama lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipangia ”
Alisisitiza Dkt. Mpango.
Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane mwaka huu ambayo ni
ya 24 kufanyika kitaifa huku yakifanyika mwaka wan ne mfululizo mkoani Lindi
inasema “Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi
wa kati”.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb), akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na
baadhi ya Taasisi zilizo chini ya Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 24 ya
Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika
viwanja vya Ngongo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) anayesaini kitabu cha wageni, katika picha ya pamoja na watumishi
wa Wizara ya Fedha alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika
viwanja vya Nanenane, Ngongo, mkoani Lindi.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara na Taasisi zake
walioshiriki Maonesho ya 24 ya Nanenane, yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja
vya Ngongo mkoani Lindi. Kulia kwake ni Meneja Takwimu Mkoa wa Lindi Bw.
Moses Sagala, kushoto kwake ni Mkuu wa Hazina Ndogo Lindi Bi. Pili Kamali, na
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware.
SHARE
No comments:
Post a Comment