TRA

TRA

Wednesday, August 2, 2017

HAYA SASA. WOLPER AFUNGUKA KUHUSU KUBADILI WANAUME

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Jacqueline Massawe ‘Wolper’.
WAKATI mashabiki wakiwa bado wanamshangaa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Massawe ‘Wolper’ juu ya tabia yake ya kubadili wanaume kila kukicha, katika hali ya kushangaza, ameibuka na kudai kuwa ataendelea kubadili wapenzi, muda wowote atakapogundua kuwa aliyenaye, hana vigezo.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Wolper alisema hawezi kuogopa maneno ya watu wanayosema juu yake kwa vile hawaelewi anachokumbana nacho katika mapenzi, kwani hawezi kung’ang’ania kukaa kwenye uhusiano ambao haendani nao au unampa shida.

Wolper na mpenzi wake, Brown.

“Unajua unapokuwa na mpenzi huwezi kujua kuna tabia utakumbana nazo ambazo haziendani na wewe, lakini pindi unapogundua ni bora kuondoka kuliko kukaa sehemu ambayo huna furaha nayo,” alisema Wolper.

Staa huyo aliongeza kuwa hata mtu aliyenaye hivi sasa endapo atagundua kama tabia hazirandani, ataangalia ustaarabu mwingine kwani haogopi kusemwa kuhusu kubadilisha wapenzi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger