
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 28, 2017 imepokea taarifa ya Mkemia
kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyoonesha kuwa sampuli ya
mkojo wa Agnes Gerald maarufu kama Masogange una chembechembe za dawa za
kulevya.
Taarifa
hiyo imepokelewa baada Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kutoa uamuzi
wake ambapo amesema Mahakama imepokea taarifa hiyo na pingamizi la
utetezi limetupiliwa mbali.
Pingamizi la upande wa utetezi ni kwamba fomu zilizopelekwa kwa Mkemia Mkuu hazikufuata sheria.
Hakimu
Mashauri amesema Mkemia huyo Elia Mulima ambaye ni Shahidi wa kwanza
ana haki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti Mahakamani.
Kuhusu
hoja ya kuwasilishwa maombi ya kupimwa mkojo Masogange, Hakimu amesema
ni wazi Polisi walipeleka maombi kwa Mkemia na mshtakiwa alienda akiwa
chini ya askari wawili, ambapo walipatiwa kontena kwa ajili ya kuweka
sampuli ya mkojo wa Masogange.




SHARE
No comments:
Post a Comment