Msanii
wa maigizo aliyefanya vizuri na filamu ya 'Mapenzi ya Mungu', Elizabeth
Michael ' Lulu' amefunguka na kusema wasanii wa maigizo bongo wanafeli
kutokana na kutojielewa ni kitu gani ambacho wanakitaka kwenye sanaa,
badala yake wanafuata mikumbo.
Lulu
amefunguka hayo hivi karibuni akizungumza na wanahabari na kusema kuwa
wasanii wengi wa Tanzania hawapendi kujishughulisha kutafuta kitu kizuri
kwa kuwa wengi wao walifuata mkumbo kwenye kuigiza na wengine
walichukulia kama sehemu ya kujipatia umaarufu ili maisha yaendelee au
sehemu ya kupotezea muda.
"Ukweli
upo kwenye uigizaji kuna watu tunachukulia hii ni kazi, wapo wanaofanya
kama sehemu ya kipaji chake lakini pia wapo ambao wanachukulia kama
sehemu ya kujipatia umaarufu au ku-refresh kwani wanakua na kazi zao
zingine, na hao ndio wanaosababisha tuonekane waigizaji wa muvi
tumefeli".
Pamoja
na hayo Lulu ameongeza, "Unajua pia kufuata mkumbo ni kitu
kilichoturudisha nyuma. Watu wengi walikuwa wanaangalia mafanikio ya mtu
mmoja na wote tukawa tunapita njia zilezile ili tufanikiwe badala ya
kutafuta za kwetu ndiyo kama mnavyoona sasa hivi tunalalamika lakini
mashabiki zetu wanatusapoti hivyo japo tunawakwaza".
Akizungumzia
kuhusu wasanii wa Nigeria walivyoweza kufanikiwa katika filamu zao,
Lulu amesema ni pamoja na upendo na ushirikiano wanaoonyeshana katika
kazi zao na kuongeza kwamba pamoja na kufanya kazi zenye ubora wa
kimataifa watu hao hawajasahau utamaduni wao.
Kuhusu
sababu za wasanii wa filamu kutokaa 'Location' kwa muda mfupi
kutengeneza filamu zao kwa usahii muingizaji Lulu amefunguka na kusema
changamoto kubwa huwa ni bajeti kwa wasanii hao.
"Bajeti
zetu ni tatizo. Bado hatujawa na uwezo wa kuweka bajeti kubwa kwenye
filamu ndiyo maana tunaomba tuwezeshwe ili tufanye kazi zenye ubora.
Kuna vitu ambavyo sisi pia tunavifanya kwa mapungufu kwa sababu hatuna
uwezo wa kumpatia pesa mtu sahihi wa kufanya kazi husika ndiyo maana
unakuta tunafanya kazi kwa uwezo wetu tu.
SHARE
No comments:
Post a Comment