Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Genius Kings Nusery& Primary School, Machage Kisyeri, (Kulia) akisoma hotuba.
Mwalimu
Mkuu wa shule, Aloyce Siame (kushoto) akimkabidhi risala Profesa Joseph
Kahamba , ambaye alikuwa mageni rasmi wakati wa mahafali hayo.Katikati
ni Mkurugenzi wa shule Julius Rutabanja.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siame (kulia) akikabidhiwa zawadi ya kikombe na Profesa Joseph Kahamba.
Paroko
msaidizi wa Roho Mtakatifu Parokia ya Segerea Velence Kisaka (kulia)
akibarikia shule hiyo baada ya kufanya ibada kwa ajili ya kuwaombea
wanafunzi wa darasa la saba wanaojiandaa na mitihani ya taifa.
Mwalimu
wa Dini ya Kiislam Shekhe Hussein Abdalah akiongoza swala kwa ajili
kawaombea watoto wa darasa la saba katika shule hiyo.
Mgeni rasmi akiangalia wanafunzi wakifanya majaribio ya sayansi.
Wahitimu wakitoa burudani kwa wazazi na wageni waalikwa.
Kikosi cha scout shuleni hapo wakifanya mambo yao
Wanafunzi wakionyesha kipaji cha kucheza ngoma za asili.
*Wahitimu waaswa kwenda na kasi ya sayansi na teknolojia
Wakati
serikali ya Tanzania inao mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda,wanafunzi wanaohitimu masomo wametakiwa kujiona sehemu ya
mkakati huo na kusoma kwa bidii kupata ujuzi wa taaluma mbalimbali
ikiwemo kutoogopa kusoma masomo ya hesabu na sayansi.
Ushauri
huo umetolewa na daktari bingwa nchini wa magonjwa ya nevu
(Neurosurgery) kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili,Profesa Joseph Kahamba,
wakati wa mahafali ya darasa la saba ya msingi ya Genius Kings
yaliyofanyika Segerea jijini Dar es Salaam .
Profesa
Kahamba alisema kuwa nchi yetu bado inakabiliwa na changamoto ya kuwa
na wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali ambapo aliwataka
wanafunzi wanaohitimu masomo na waliopo mashuleni na vyuoni kujipanga
kuhakikisha wanapata utaalamu wa fani mbalimbali tayari kwa kutumikia
taifa la Tanzania.
“Wanafunzi
waliopo mashuleni na vyuoni mnapaswa kujipanga kwa kuhakikisha mnasoma
kwa bidii na kupata ujuzi wa fani mbalimbali kwa kuwa mapinduzi ya
kuendeleza taifa letu yanayoendelea yanahitaji wataalamu wa fani
mbalimbali na wanaotegemewa kuchukua majukumu hayo hawatoki nje ya nchi
bali ni nyinyi vijana wa kitanzania”Alisema Profesa Kahamba.
Aliongeza
kusema kuwa kinachotakiwa kwa wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni
kujibidisha kusoma kwa bidii na kupata taaluma za fani mbalimbali na
wahakikishe wanajiamini na kuhakikisha ndoto zao walizojiwekea zinatimia
na wanakuwa na uzalendo wa kuitumikia nchi na kuleta maendeleo chanya
katika jamii kupitia elimu waliyoipata.
Profesa
Kahamba aliupongeza uongozi wa shule ya Genius Kings kwa kufanya
uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kuwa umelenga kuunga mkono jitihada
za serikali za kuboresha elimu nchini na kuleta mabadiliko wenye jamii
kwa kuwa elimu ni njia pekee ya kuleta maendeleo kwa haraka katika
ujenzi wa taifa . “Naupongeza uongozi wa shule kwa kuwekeza katika elimu
na nawapongeza wazazi ambao wanawekeza katika elimu kwa kusomesha
watoto wao maana elimu bora katika jamii inachangia kuleta mabadiliko ya
nchi haraka”.Alisema
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo Bw. Aloyce Siame, alisema kuwa katika kipindi cha
miaka 10 tangu shule ianzishwe imeweza kushikilia rekodi ya kufanya
vizuri kwa kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba na la nne kwa kiwango
cha juu na kuingia katika shule tano bora wilayani Ilala na shule bora
20 mkoani Dar es Salaam mfululizo hali ambayo imewajengea hari ya kuzidi
kufanya vizuri kwa mwaka huu na miaka ijayo.
“Moja
ya mtazamo wa shule hii ni kuifanya kuwa shule bora ya mfano inayotoa
elimu bora nchini kuanzia shule ya awali na shule ya msingi na
sekondari.”Tumejipanga kuhakikisha lengo hili linatimia na tunatoa
shukrani kwa serikali,wazazi na wadau wote ambao wameonyesha kutuunga
mkono katika kipindi hiki cha awamu ya kwanza ya mwanzo ya miaka 10 na
kuwezesha mafanikio haya kupatikana”.Alisema.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi mkuu wa shule hiyo ,Bw.Machage
Kisyeri,aliwapongeza wahitimu kwa kufikia hatua hiyo na aliwataka
watumie elimu waliyoipata kujipanga zaidi kwa masomo ya sekondari ambayo
yanawakabili mbele yao. “Maisha sio lelemama mnapaswa kupambana zaidi
katika hatua inayofuatia na kuhakikisha msingi wa elimu imara
tuliyowapatia unawaongoza kuelekea katika kupata mafanikio ya kitaaluma
popote pale mtakapokwenda”Alisisitiza.
Aliongeza
kuwa shule imejizatiti kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha
elimu nchini ambapo kuanzia mwezi Januari mwakani itaanza kutoa elimu ya
sekondari katika shule yake mpya iliyojengwa sehemu ya Mataya wilayani
Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Kuhusiana
na changamoto wanazokabiliana nazo alisema kuwa zipo changamoto za
kawaida kinachotakiwa ni ushirikiano baina ya wazazi,walimu,na wadau
wanaosimamia elimu ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana na elimu ya
Tanzania inazidi kupanda “Walimu wakiwezeshwa vizuri na kupewa
ushirikiano wa kutosha naamini shule nyingi za Tanzania zitatoa elimu
bora kwa kuwa tunao walimu wengi wazuri ambao wakitumiwa ipasavyo
tutasonga mbele”.Alisema.
SHARE
No comments:
Post a Comment