TRA

TRA

Monday, August 7, 2017

Majimarefu: Magufuli ameletwa na Mungu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (CCM) maarufu kama Profesa Majimarefu amesema Rais John Magufuli ameletwa na Mungu.

Akizungumza mjini Korogwe, Majimarefu alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa miaka 10 ya Rais Magufuli haitoshi na kutaka uongezwe zaidi.

"Wewe umeletwa na Mungu, miaka 10 haikutoshi, uongozwe. Unafanyakazi hakuna haja ya kubadilisha badilisha," alisema.

Alionesha kufurahishwa na hatua ya Rais kutoa kibali mara mbili cha kumruhusu kusafiri kwenda nje kwa ajili ya kutibiwa/

"Namshukuru sana Rais" alisema na kutumia nafasi hiyo kumuomba Rais awatengenezee barabara ya lami kwani bado kuna kizungumkuti huku akiomba mashamba ya katani yatazamwe upya.

Watu mbalimbali wamekua na maoni juu ya utendaji kazi wa Rais Magufuli akiwemo pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, wananchi na hata baadhi ya wabunge bungeni walisikika wakisema wanatamani Rais huyu atawale kwa muda mrefu.

Hata hivyo, leo wakati Rais Magufuli akiwa kwenye ziara yake Tanga amenukuliwa akijibu hicho kinachosemwa kuhusu yeye kuendelea kukaa madarakani hata baada ya muda wake kumalizika.

Rais Magufuli alisema hawezi kukaa madarakani kwenye urais kwa miaka 20 kama alivyoombwa pia na Mbunge Ngonyani kwa sababu ni kinyume cha Katiba.












Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger