Mshambuliaji wa
Klabu ya Fc Monaco, Kylian Mbappe anatarajiwa kukamilisha usajili wake
wa mkopo na klabu ya Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG).
Kituo cha redio cha Ufaransa siku ya Jumapili kiliripoti kuwa PSG wamekubali kulipa euro milioni 180 ambazo sawa na dola za marekani 215,000,000) ikiwa ni pamoja na mafao kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 18.
Kylian Mbappe (kulia)
Usajili huo utaweka historia katika uhamisho kuwa usajili wa pili wa gharama kubwa zaidi katika soka baada ya Neymar, ambaye alijiunga na PSG kutoka Barcelona kwa euro milioni 222 mapema mwezi huu.
Hata hivyo kuna wasiwasi zaidi kuhusiana na kile kilicho juu ya mkutano wa UEFA wa Fedha unaohusu gharama kubwa katika usajili wa wachezaji Fair Play (FFP) na ndio maana PSG wanataka kwanza kumsajili kwa mkopo Mbappe .
Monaco na PSG siku ya Jumapili zilifikia makubaliano ya Kylian Mbappe kwenda PSG kwa gharama ya usajili wa euro milioni 180.
SHARE
No comments:
Post a Comment