Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza
jambo wakati wa hafla fupi ya kuwapokea wanamichezo wanafunzi waliotoka
kushiriki mashindano ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki
(FEASSA) leo Agosti 30, 2017, Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja na Mratibu wa Michezo Shule ya Sekondari
Makongo Kapteni Abdul Mbaruka Tika.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea
bendera ya taifa kutoka kwa Kapteni wa timu ya wanafunzi wa Sekondari za
Tanzania walioshiriki mashindano ya michezo kwa Shule za Sekondari za Jumuiya
ya Afrika Mashariki (FEASSA) katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Idara
ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu
wa Msafara wa timu ya wanafunzi wa Sekondari za Tanzania walioshiriki
mashindano ya michezo kwa Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki
(FEASSA) Mwl. Vitalis Shija akielezea jambo mbele ya Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto)
wakati wa hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini
Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Alex
Nkenyenge na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT). Mohamed Kiganja.(PICHA NA: FRANK SHIJA – MAELEZO).
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpongeza
mmoja wa mwanamichezo aliyeibuka mshindi wa tatu katika riadha kwenye mashindano ya FEASSA, Winfrida Makenji
wakati wa hafla fupi ya kuwapokea wanamichezo hao waliotoka kushiriki
mashindano ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSA) leo
Jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment