Mwanariadha wa Botswana,
Isaac Makwala atajiunga na mwanariadha wa Afrika Kusini, Wayde van
Niekerk, katika kuwania ubingwa wa dunia wa fainali ya mita 200 baada ya
kukimbia pekee yake na kufuzu huko London jana.
Makwala
alikosa kushiriki mbio za siku ya Jumatatu alipozuiwa kushiriki na
maafisa, kufuatia mlipuko kwa ugonjwa unaojulikana kama norovirus. Aliruhusiwa kukimbia hiyo jana ambapo alikimbia muda wa sekunde 20.20 peke yake na kufanikiwa kufuzu.
Mwanariadha raia wa Marekani Isiah Young alishinda nusu fainali ya kwanza kwa sekunde 20.19 huku muingereza Mitchell-Blake akimaliza wa tatu kwa sekunde 20.19
Nilikuwa tayari kukimbia mita 400 peke yangu - Makwala
"Bado nimevunjika moyo," alisema Makwala.
" IAAF wangeniruhusu nikimbie mbio za miata 400. Nilikuwa tayari kukimbia mita 400 peke yangu ndio nikimbie mita 200.
"Mbio za mita 400 ndizo ninajifunza.
Awali makwala alikimbia peke yake katika laini ya saba, na kufuzu kwa njia rahisi.
Baada ya kukosa kukimbia mbio za kufuzu za mita 200 na fainalia ya mita 400, IAAF ilimpa Makwala fursa nyingine ya kukimbia mita 200 baada ya kupata barua kutoka kwa shirikisho la riadha la Botswana.
SHARE
No comments:
Post a Comment