TRA

TRA

Monday, August 28, 2017

ODINGA, KENYATTA, WAANZA KUPAMBANA MAHAKAMA KUU YA KENYA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 




MAJAJI Saba wa Mahakama Kuu nchini Kenya, wameanza kusikiliza pingamizi la Muungano wa upinzani NASA, chini ya aliyekuwa mgombea wa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya, Raila Odinga, kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambapo mgombea wa Jubilee, Rais Uhuru Kenyatta, aliibuka mshindi.
Mahakama hiyo tayari imekubali baadhi ya maombi ya NASA, ya kutaka mfumo wa IT wa 34A
Pia Mahakama hiyo imeamuru IEBC kutoa nyaraka (fomu) namba 34A, B na C.
Jopo la mawakili wa NASA, likiongozwa na James Orengo, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Amos Wako, Otiende Amollo na Moses Watangula, linataka Mahakama Kuu ya Kenya, itengue matokeo yaliyompa ushindi Rais Kenyatta.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger