TRA

TRA

Saturday, August 5, 2017

Rais Paul Kagame ashinda kura nyingi Rwanda

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.

Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. 

Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba. 


 Kagame alipiga kura mjini Kigali
Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa.

Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana 

Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.

Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.
Wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa ndiyo imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura.

Hata hivyo chama tawala kimekana madai hayo.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger