Ndege moja ya
Ufaransa iliyokuwa na abiria 330 ilikuwa kilomita 100 pekee na kombora la
masafa marefu lililorushwa na Korea Kaskazini, maofisa wanasema.
Kampuni ya Airfrance inasema kuwa ndege yake haikuwa hatarini lakini imejiweke marufuku ya kusafiri katika anga ya Korea Kaskazini kama tahadhari.
Pentagon inasema kuwa kombora hilo lilipaa katika anga yenye shughuli nyingi.
Kombora la Korea Kaskazini lilikaribia ndege ya Ufaransa
Maafisa wa Marekani nara kwa mara wamekuwa wakionya kuhusu hatari zinazoletwa na makombora dhidi ya ndege za abiria katika eneo hilo.
Njia iliotumiwa na ndege hiyo aina ya Boeing 777 inaonyesha kuwa ilikuwa magharibi, mwa Hokkaido, kaskazini mwa taifa la Japan , wakati bora hilo la Korea Kaskazini lilikuwa hewani.
Japan na Marekani inakadiria kwamba kombora hilo lilianguaka kati ya kilomita 100na 150 karibu na ndege hiyo.
"Kombora hilo liliruka katika anga na kuanguka nchini Japan, eneo ambalo hutumika na vyombo vya kibiashara na vile vya uvuvi,"alisema msemaji wa Pentagon Jeff Davis.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment