Kaimu katibu mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka
akisalimiana na viongozi wa chama mkoa wa kaskazini unguja akiwa katika
ziara ya kikazi visiwani Pemba.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka
akipokelewa na viongozi ofisi za CCM wilaya ya micheweni katika ziara
ya kikazi visiwani Pemba.
Vijana wakiburudisha kwa kupiga dufu wakati wa mapokezi ya Kaimu katibu
mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shakaalipowasili ofisi za
CCM wilaya ya micheweni katika ziara ya kikazi visiwani Pemba.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka wa pili
kulia pamoja na mkuu wa idara ya Uchumi uwezeshwaji na fedha
(UVCCM)Dorice Obedi wakisain Vitabu vya wageni walipowasili wasili
katika ofisi za CCM Wilaya ya micheweni ziara ya kikazi visiwani Pemba.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka
akizungumza jambo pamoja na mwl,Ally khatibu Hassan Mkuu wa shule ya
msingi Michekweni wakati akikagua jengo la Ujenzi wa maktaba pamoja na
madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni wakati wa ziara ya kikazi
visiwani Pemba.
Wanafunzi wa Darasa la kwanza Issa Haji (wa kwanza kulia) pamoja na
Abdulwahid abdallah wakisalimiana na Kaimu katibu mkuu wa umoja wa
Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka wakati alipokwenda kukagua jengo la
Ujenzi wa maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akimfunga
Vifungo vya shati Mwanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi
Micheweni Abdulwahid abdallah wakati alipokwenda kukagua jengo la
Ujenzi wa maktaba pamoja na madarasa ya Shule ya Msingi Micheweni.
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa Shumba mjini akikagua sehemu itakayojengwa jeti
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akigagua
ujenzi wa ofisi ya ccm tawi la njuguni inayojengwa na mwakilishi Jimbo
Afisa mipango wa halmashauri ya konde (pili kushoto)akitolea ufafanuzi
juu ya ujenzi wa soko la mboga mboga la samaki pamoja na mbogamboga kwa
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwa
katika ziara ya kikazi visiwani Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg
Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Viongozi na wanachama wa CCM na
Jumuiya zake Tawi la kuiyu Mbuyuni akiwa katika Ziara ya Kikazi Mkoa wa
Kaskazini Pemba .
Wanachama Wa CCM na Jumuiya zake wakishangilia katika mkutano wa ndani uliofanyika Skuli ya Michekweni.Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ustadh,Abdul mohammed akifungua kwa Kusoma quran Tukufu katika ukumbi wa Skuli ya Michekweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mkuu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha (UVCCM) ndg:Dorice Obed
akizungumza katika Mkutano wa ndani wa Wanachama na Viongozi wa CCM na
Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Abeid Juma Ally akizungumza
Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka
akizungumza katika Mkutano wa ndani wa Wanachama na Viongozi wa CCM na
Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni Mkoa wa Kaskazin Pemba.
Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Michekweni wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha ndg:Dorice Obed akicheza
nyimbo ya CCM pamoja na wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake
Wilaya ya MichekweniMkoa wa Kaskazin Pemba
''Shaka ni kijana jasiri mwenye kujenga hoja na kushambulia wapinzani
kwa Vielelezo hamofii Seif,Sumaye Lowasa na wengine,wala
kingunge,anwajibu kwa ushahidi na Vielelezo''Alisema Dady faki Dady
msaidizi wa Rais SIASA Pemba wakati akizungumza katika mkutano wa ndani
uliofanyika Skuli ya Michekweni.Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA ZOTE NA
FAHADI SIRAJI)
********
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa Jukumu la
kuleta maendeleo ya kiuchumi katika jamii ni la kila mwananchi sio
jukumu la serikali pekee.
UVCCM imesema kuwa jukumu la serikali ni kuwaonyesha wananchi fursa
zilipo na namna bora ya kuzichanganua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi
ili kukuza uchumi wa mtu mmoja
mmoja na jamii kwa ujumla wake sambamba na kuwezeshwa kupata mikopo katika vikundi vyao vya ujasiriamali.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka jana Agosti 16, 2017
alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya
zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri
Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kuwa vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kutumia nguvu
zao vizuri kwa kufanya kazi ili kujikwamua kiuchumi katika familia zao
badala ya kukaa maskani kujadili mambo yasiyokuwa na tija kwao.
Aliongeza kuwa UVCCM inaunga mkono vijana kukaa maskani kwa maslahi
mapana ya mjadala wa Maendeleo yatakayopelekea kujikwamua kiuchumi ikiwa
ni pamoja na kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali.
Shaka alisema kuwa Kila mwananchi kwa nafasi yake anatakiwa
kuwajibika kwa nafasi aliyonayo ndani ya chama ama serikali kwani
wananchi wanataka maendeleo ya uchumi wao sio ahadi hewa za majukwaani.
Aidha, alisema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Dkt John Pombe Magufuli ipo pamoja na watanzania wote ambao ni
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ama wale ambao sio wanachama wa vyama
vya siasa kwani mchakato wa maendeleo hauangalii itikadi za vyama vya
siasa.
Alisema wananchi wanatakiwa kutumia Tunu ya amani, umoja na mshikamano
uliopo nchini kufanya shughuli za maendeleo na kujiepusha na maneno
ambayo yataleta chokochoko za kuondoa mshikamano katika jamii.
Shaka alisema kuwa vijana wanatakiwa kujiajiri katika ujasiriamali kwa
kuchukua hatua za makusudi za kujiajiri kwani kusubiri ajira za serikali
zitawachelewesha na pengine kufikia hatua ya uzee pasina kuajiriwa
kutokana na uchache wa ajira serikalini na wingi
wa vijana.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM ameanza ziara ya kikazi juzi Agosti 15, 2017 visiwani
Pemba ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.
Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba
SHARE
No comments:
Post a Comment