
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto), akikaribishwa
na Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Machechu katika sherehe za
maadhimisho ya miaka 50 ya Benki jijini Dar es Salaam juzi. Wa pili
kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango , Dk. Ashatu Kijaji na
Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe (kulia).

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto), katika sherehe za maadhimisho ya
miaka 50 ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam juzi. Wengine kutoka kulia
ni Waziri Mkuu wa zamani, Dk. Salim Ahmed Salim na Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu
Hassan (katikati), akipiga picha ya pamoja na kutoka kushoto; Mjumbe wa
Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein; Spika, Job Ndugai; Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango , Dk. Ashatu Kijaji; Mwenyekiti wa Bodi ya NBC,
Nehemiah Mchechu; Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr.
Bernard Kibesse na Waziri Mkuu wa zamani, Dk. Salim Ahmed Salim.

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC,
William Kallaghe (kulia), akiwaongoza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu
Hassan (katikati) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango , Dk. Ashatu
Kijaji (kushoto), walipokwenda katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50
ya benki hiyo ambapo makamu wa rais alikuwa mgeni rasmi. Wa pili kulia
ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu. Sherehe hizo zilifanyika
jijini Dar es Salaam juzi.

Meneja Mahusiano wa NBC, William
Kallaghe akitoa maelezo kwa njia ya picha kwa Makamu wa Rais, Mama Samia
Suluhu Hassan (wa tatu kulia), kuhusu historia ya benki hiyo tokea
ilipoanzishwa wakati wa sherehe hizo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
Bodi ya benki hiyo, Nehemiah Mchechu na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
, Dk. Ashatu Kijaji.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu akizungumza katika sherehe hizo.

Spika wa Bunge ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akizungumza.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango , Dk. Ashatu Kijaji akizungumza.

Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mama
Samia Suluhu Hassan akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50
ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam juzi.

Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu akikabidhi zawadi kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu
Hassan (katikati), akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
, Dk. Ashatu Kijaji katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Benki
ya NBC jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC,
Nehemiah Mchechu.

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu
Hassan (kulia), akimkabidhi zawadi kwa Arnold Kilewo mmoja wa
viongozi wa bodi ya zamani ya NBC katika hafla hiyo. Katikati ni
Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu.

Mwanamuziki mashuhuri wa Afrika
Kusini, Yvonne Chakacha (kulia), akisakata rumba na Mkurugenzi Mtendaji
wa NBC Tanzania, Theobald Sabi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50
ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
, Dk. Ashatu Kijaji akiagana na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim
Hussein mara baada ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya benki hiyo
jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC,
Nehemiah Mchechu, Meneja Mahusiano, William Kallaghe (kulia) na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi.

Mwanamuziki mashuhuri wa Afrika
Kusini, Yvonne Chakacha (kushoto), akitoa burudani katika sherehe za
maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya NBC hiyo jijini Dar es Salaam juzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa
NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akisalimiana na viongozi wa NBC, kutoka
kushoto, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Theobald Sabi, Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.
SHARE
No comments:
Post a Comment