Kikosi cha Kocha Joseph Omog
kinatarajiwa kuteremka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumapili kumenyana
na Singida United katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na mchezo wa Ngao
ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga Agosti 23 mwaka huu mchezo
huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa kumi na mbili jioni.
Huo utakuwa mchezo wa nne wa kirafiki kujiandaa na msimu mpya
kwa kikosi cha kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya awaki
kushinda mechi moja, sare moja na kufungwa katika mechi zake tatu
zilizotangulia.
Na utakuwa mchezo wa kwanza kucheza naa timu ya nyumbani, kwani
mechi zilizopita ilifungwa 1-0 na wenyeji Orlando Pirates kabla ya
kutoa sare ya 1-1 na Bidvest katika ziara ya Afrika Kusini na Jumanne
ikashinda 1-0 dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Uwanja wa Taifa.
Kwa Singida United itakuwa
inacheza mechi ya pili ndani ya wiki moja Uwanja wa Taifa, kwani
Jumamosi iliyopita ilifungwa 3-2 na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania, Yanga licha ya kuongoza kwa mabao 2-1 hadi mapumziko.
Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm anaamini kucheza na vigogo
wa Tanzania, Simba na Yanga kabla ya kuingia kwenye Ligi Kuu ni kipimo
kizuri na Jumamosi atakamilisha mpango wake.
Pamoja na kwamba imepanda Ligi Kuu msimu huu, lakini Singida
United inatarajiwa kufanya vizuri katika ligi hiyo baada ya usajili wa
wachezaji nyota kutoka mbalimbali maarufu, wakiwemo wa saba wa kigeni.
SHARE
No comments:
Post a Comment