Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro imesema picha ambazo zinamuonyesha simba jike
akimnyonyesha mtoto wa chui ni moja kati ya matukio ya ajabu ambayo
yanatokea katika hifadhi hiyo.
Picha
hizo ambazo zilisambaa katika mitandao ya kijamii na kuibua gumzo huku
wengi wakishangazwa na kitendo hicho kisicho cha kawaida katika
ulimwengu huu.
Kwa
mujibu wa BBC wanyama hao walionekana na Joop Van Der Linde mgeni
katika katika eneo la Ndutu safari Lodge nchini Tanzania katika eneo la
uhifadhi la wanyama pori la Ngorongoro.
Akiongea
na Bongo5, Afisa Hifadhi wa Ngorongoro, Peter Makutian, alisema tukio
hilo huwenda ni kweli limetokea katika hifadhi hiyo kutokana na matukio
mengi ya ajabu ambayo yamekuwa yakitokea katika hifadhi hiyo.
“Ngorongoro
kuna mambo mengi sana ambayo hata ukisimuliwa nje hauwezi kuamini, kama
hilo tukio la Simba kumnyonyesha mtoto wa chui ni matukio ambayo ni
magumu kutokea katika maisha ya wanyama hao lakini likitokea linakuwa ni
tukio la kishistoria,” alisema Peter.
Aliongeza,
“Kama nilivyosema hatuna taarifa rasmi lakini wengi ambao wameona hiyo
picha wanasema ni Ngorongoro, ile picha siyo ya kutengenezwa na kama
unavyojua Ngorongoro pia ni makazi ya watu kwahiyo kuwenda kati ya watu
ambao wanaishi pale walishuhudia tukio hilo na kuamua kulipiga picha au
wagon ambao wanakuja kila siku, lakini kwetu sisi hilo ni tukio la
ajabu sana kwa sababu wanyama hawa hawapiki chungu kimoja, kila mmoja
anamaisha yake na tabia zake ingawa ni wanyama ambao wapo kwenye kundi
moja la wanyama wala nyama,”
“Lakini
yapo matukio ambayo yatokea kwa nadra na katika mazingira ya
kustajabisha kama tukio hilo lakini ndani ya Ngorongoro kuna matukio
mengi ya namna hiyo. Kwa mfano katika maisha ya Simba na Chui hawa ni
wanyamba ambao kila mmoja anaweza akamuua mwenzake lakini hamli, lakini
ndani ya Ngorongoro Simba walimuua chui na kumla kitu ambacho si
chakawaida kutokea katika maisha ya hawa wanyama,” alifafanua zaidi
Peter.
Kwa
upande wa Balozi wa Ngorongoro, Mrisho Mpoto amesema yeye kama balozi
katika kipindi hiki cha Nane Nane amewataka wakazi wa Arusha
kuchangamkia ofa iliyotolewa na Ngorongoro ya kutembelea hifadhi hiyo
kwa tsh 50,000.
“Huu
ni wakati wa kila mtu kwenda Ngorongoro, hii ni fursa nzuri kwa wakazi
wa Arusha kwa sababu kama mlivyosikia ni elfu 50000 tu. Hiyo ni kwaajili
ya chakula, usafiri pamoja na mtu ambaye atakuongeka katika kila
sehemu. Kwahiyo kweye hili mimi naona hii ni fursa nzuri kutoka
Ngorongoro ambapo kuanzia kesho tarehe 6 tripu ya kwanza na kuendelea
tarehe 7 na 8,”
SHARE
No comments:
Post a Comment