Na Agness Moshi na Bushiri Matenda –MAELEZO.
Watanzania
na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya nchini wameombwa kuendelea
kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili iendelee kufanya
kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora.
Hayo
yamesemwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mwenyekiti wa Mfuko wa Tulia Trust Mhe.Tulia Akson, wakati akikabidhi
msaada runinga nne na katoni mbili za maziwa vyenye thamani ya
shilingi 1,000,000 vilivyotolewa kwa watoto waliopo kwenye Taasisi
hiyo kwa ushirikiano na Dstv, TSN na Kampuni ya Twincity.

Dkt.Tulia
amesema msaada wa runinga unatimiza ahadi waliohaidi kwa taasisi hiyo
na unamaana kubwa sana kwa sababu utawasaidia watoto wanaokaa
hospitalini hapo kwa muda mrefu kujifunza ,na kuwaburudisha kwa
kipindi chote cha matibabu ya awali kabla ya kufanyiwa upasuaji.
“Watoto
hawa wanakaa muda mrefu hospitalini wakitibiwa hivyo wanashindwa
kujumuika na wenzao kwa michezo jambo ambalo linawafanya wahisi upweke
kwa kuwapatia runinga kutawasaidia kuondoa hali hiyo , kuwaburudisha na
kuwapa nafasi ya kujifunza kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na
king’amuzi cha DSTV”, alisema Dkt.Tulia
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt.Mohammed Janabi amesema kuwa si watoto
tu watakaofaidika kwani hata wazazi wao wataweza kujua mambo mbalimbali
yanayoendelea Nchini kwa kuangalia taarifa za Habari zitakazokua
zinaonyeshwa kupitia chaneli mbalimbali.
“
Sio watoto wote wanaokuja hapa wanatatizo la moyo peke yake wengine
wanakuja wakiwa na Magonjwa mengine ambapo inabidi tuanze kuwatibia
kwanza magonjwa hayo ambapo wakati mwingine yanachukua muda mrefu hivyo
basi kwa kipindi chote hicho runinga hizi zitakua zikiwapa burudani,
elimu kwa masomo mbalimbali kama vile kiingereza, hesabu kwa watoto
wakubwa na kwa wale wadogo wataburudika kupitia katuni”,alisema
Dkt.Janabi.
Dkt.Janabi
ameongeza kuwa msaada wa maziwa waliopewa utasaidia kuimarisha afya za
watoto wadogo wanaotibiwa kwani wapo wengine wamekuja wakiwa na Afya
duni ,wengine wana magonjwa ya utapia mlo hivyo kupelekea kuchelewa
kupatiwa matibabu.
Aidha,Dkt.Janabi
amemshukuru Dkt.Tulia kupitia Mfuko wake wa Tulia Trust kwa kuendelea
kuhamasisha wadau mbalimbali kuipatia misaada Taasisi hiyo.
Kwa
upande wake mtoto Mwamvita Hassani mwenye umri wa miaka 13 kutoka
wilayani Kondoa kwa niaba ya watoto wanaotibiwa kwenye Taasisi hiyo
ametoa shukrani zake kwa Naibu Spika na wadau waliowapa misaada hiyo.
“Ninawashukuru sana kwakutuletea Tv na Maziwa,Tumefurahi na tunawaombea watuletee Tv zingine”, alisema Mwamvita.
Dkt.Janabi
amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia upatikanaji wa vitanda
kwa ajili ya Taasisi hiyo kwani wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo swala la upungufu wa vitanda kwa wagonjwa kwani wanavitanda 128
tu ambavyo havikidhi mahitaji kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa
wanaofika kwa ajili ya matibabu.
SHARE













No comments:
Post a Comment